Azimio la Uhuru 2020-03-16
±âÀÚ | À̸ÞÀÏ Á¶È¸¼ö 295  ´ñ±Û 0
 
Kwa maneno na vitendo tunatangaza kwamba Korea ni nchi huru na Wakorea ni wenye moyo thabiti wa kujitegemea. Kwa kulifanya tangazo hili lijulikane kwenye nchi zote duniani, tunaazimia kudhihirisha usawa wa binadamu wote na kuwawezesha Wakorea wa vizazi vijavyo kuwa na uwezo wa kudumisha haki zao za kujikimu. Tangazo hili linafanywa kutokana na fahari ya kitaifa yenye miaka elfu tano. Tunatangaza hivi kulingana na utiifu imara miongoni mwa wananchi milioni ishirini. Tangazo hili limekusudiwa kutimiza maendeleo ya uhuru yaliyoendelea daima. Tunafanya azimio hili la uhuru kuendana na wakati wa fursa na hatima ya ujenzi wa dunia mpya unaotokana na unyofu wa binadamu wote. Hii ni amri ya Mwenyezi Mungu na mkondo mkuu. Azimio hili ndilo sauti ya haki ya binadamu wote. Kwa hivyo hakuna lolote linaloweza kuzuia mkondo huu mkuu.

Tayari miaka kumi imeshapita tangu tulipolazimishwa kutoa mhanga kwa jina la uvamizi na ukandamizaji ambao ni urithi wa nyakati zilizopita. Katika hali hii wananchi wenzetu wameshrutishwa kudhulumiwa na kuteswa baada ya miaka elfu kadha wa kadha yenye amani na utulivu. Chini ya mfumo huu wa ukandamizaji na dhunubu, wadhalimu wamenyakua kiasi gani cha haki za kufurahia maisha yetu, wamechelewesha mwendelezo wetu wa kutafakari, wameshusha hadhi na heshima yetu na wametunyima nafasi yetu ya kuchangia maendeleo ya kiutamaduni kwa kutumia hekima na ubunifu wetu.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya maelfu ya miaka mingi, watu wetu kwa miaka kumi iliyopita waliteseka chini ya utawala wa mgeni, udhalimu na ukandamizaji, ambao ndio urithi wa nyakati zilizopita. Je, ni kiasi gani cha haki yetu ya maisha kimenyonywa? Ni kiasi gani cha maendeleo yetu ya kiroho kimezuiliwa? Je, ni kiasi gani cha heshima na hadhi zetu zimekiukwa? Na ni kiasi gani wametunyima nafasi yetu ya kuchangia katika maendeleo ya kitamaduni ya dunia na maono yetu mapya kwa kutumia hekima na ubunifu wetu imepotea?

Lililo muhimu na nyeti zaidi ni kuhakikisha uhuru wetu ili kuepukana na hisia hii ya uhasama, kutatua hali za kusumbuliwa na mateso na dhuluma, kuondoa matishio ya mustakabali, kuinua kiwango cha fahari na maadili ya taifa yaliyoaibishwa, kutorithi uhalisi unaotuaibisha kwa vijana wa kizazi kipya na kudumisha furaha na ufanishi endelevuu kwa watoto na wajukuu wetu. Wakati huu Wakorea wapatao milioni ishirini wanaficha kisu cha kisasi moyoni mwao, nguvu za kijeshi na unyofu wa kibinadamu unaoitwa dhamiri njema na moyo mwema wa kusuhubiana unasaidiana kwa haki za binadamu tunaweza kuwashinda wote wenye nguvu zaidi kushinda wengine na tutatimiza ndoto yetu yoyote ile. Tukiwa na ari na kuthubutu kwenda mbele, nani atatusimamisha kufanya hivyo na jambo gani lisilowezekana?

Kama Tutaujulisha ulimwengu malalamiko yetu ya zamani, kujikomboa wenyewe kutokana na mateso yetu ya sasa, kuondoa vitisho vya siku za usoni, na kuendeleza heshima yetu ya taifa, ili kukuza tabia ya raia binafsi, ili kuzuia watoto wetu kutoka katika urithi wa aibu, ili kuwahakikishia maisha kamili na yenye furaha kwa ajili ya uzao wetu, kazi yetu ya kwanza ya haraka ni kulinda uhuru wa watu. Leo, mioyo ya wakorea wapatao milioni ishirini ni wakfu kwa ajili ya kufikia lengo hili, na asili ya binadamu na hisia ya umri kuchanganya na majeshi ya haki na sheria ya maadili yatatusaidia. Hakuna kizuizi chenye nguvu sana kwetu kuvunja malengo haya na hakuna jambo lisilowezekana.

Hatuna nia yoyote ya kulipiza kisasi kwa Japani kwa kuvunja mkataba wa urafiki uliotiwa saini mwaka wa 1876 wala hatuna kusudio la kuikaripia Japani kwa upungufu wa uadilifu na wa uaminifu. Hatuna nia ya kuwakosoa wale wataalamu na wanasiasa wa Japani ambao wamezifanya kazi zilizorithishwa kimapokeo kutoka kizazi kimoja hadi kingine ziwe za kikoloni, kutuangalia Wakorea kama washenzi wakijifurahia kuwa washindi na kudhalilisha msingi wetu imara wa kijamii na usafi wa moyo wa taifa letu. Kwa kuwa tunajikosoa na kujitilia moyo hatuna nafasi ya kuwalaumu wengine. Kwa kuwa tunahaha kujizatiti kukabiliana na mambo yaliyo mbele yetu hatuna nafasi ya kulipiza kisasi kwa mambo mengi yaliyojiri na kuyasahihisha mambo haya. Wajibu mkubwa tulio nao sasa ni kujinyosha kimaadili na hatukusudii kuwaharibu wala kuwaumiza wengine. Garadhi yetu kuu inatuhimiza tusimame kidete mbele ya hatima yetu. Aidha hatunuii kuwa na kijicho wala uhasama kwa machukio na uhasama tuliokuwa nao.

Nia yetu ni kuwasaidia wanasiasa wa Japani waliopitwa na wakati na wenye upungufu wa fikira nyofu kwa kuwaongoza kwenye mawazo razini nguzo kuu za maisha ya kibinadamu. Tangu mwanzo muunganisho wa Korea na Japani haukutokana na matakwa ya wananchi wa mataifa haya mawili. Kotokana na sababu hizi yale maslahi ya wananchi wa mataifa haya mawili yamekuwa chao cha dhuluma, utovu wa maadili ya kiutu na takwimu bandia. Hali hii imesababisha hali ya kutotangamana vyema baina ya mataifa haya mawili na ongezeko kubwa la uhasama. Yatubidi kurekebisha makosa haya kwa ari na mori na kuumba hali mpya ya kupitia kufahamiana na kuhurumiana kwa moyo mkunjufu. Yatubidi kufahamu vizurii kwamba kufanya huku kutakuwa njia ya mkato kwa kuondoa hasara na kutuletea baraka. Kuwadhulumu Wakorea milioni ishirini wenye uhasama na hasira kwa nguvu si njia rahisi ya kudumisha amani katika eneo hili la Mashariki ya Mbali. Kufanya huku kutawahamasisha Wachina wapatao milioni mia nne wawe na hofu na kijicho dhidi ya Japani kwa kiasi cha kuhatarisha usalama katika eneo ya Mashariki ya Mbali. Litakalojiri kwa hakika ni kwamba eneo zima la Masharikia ya Mbali ni baa la kuangamizwa. Uhuru wa Korea utahakikisha Wakorea waweze kuleta uendelevu wa maisha na ufanisi unaofaa. Uhuru huu pia utawafanya Wajapani pia wajiepushe na njia mbaya na kuwapatia fursa nzuri ya kuchukua majukumu ya kuimarisha amani. Uhuru wa Korea utawafanya Wachina wasiwe na woga na wahaka wa maisha yao. Waaidha uhuru wa Korea utahakikisha amani ya eneo la Mashariki ya Mbali ambayo inahusiana moja kwa moja na amani ya dunia na furaha ya binadamu wote.

Hili haliwezi kuwa suala la mfundo au dukuduku. Dunia mpya imeshapanuka. Nyakati za nguvu za mabavu zimeshapita, na sasa nyakati mpya za maadili zimewadia. Nuru ya utu ulioimarishwa na kuthibitishwa wakati wa karne zilizopita umeanza kunururisha mwanga murua wa utamaduni kwenye historia ya binadamu.

Tumejikuta katika kipindi hiki cha marejesho na ujenzi mpya, na wanaoendesha na wimbi la mabadiliko ya dunia, hatutasita, wala hatutaogopa kukamilisha Malengo yetu. Lazima tulinde haki zetu na uhuru, na kutafuta furaha ya maisha kamili. Ni wajibu wetu kuonyesha nguvu zetu za ubunifu za asili, kudhirihisha na kufikia utukufu wa kiroho wa watu wetu katika ulimwengu uliojazwa na chemchem. Kwa sababu hii tumeamshwa.

Tutafurahia furaha tele ya maisha kwa kuhifadhi haki za uhuru na kuchipusha utamaduni wa taifa letu utakaon¡¯gara kila mahali kwa kurutubisha ubunifu wetu wa kipekee. Kwa kutimiza malengo haya tutapambana dhidi ya mambo yanayochelewesha kuchipuka kwa utamaduni wetu. Uadilifu uko nasi na ukweli unakwenda nasi. Wazee na watoto, wanawake na wanaume watajitahidi kila njia kuufanya ufufuo wenye nyemi na uchangamfu uwe uhalisi. Mababu zetu walio mzimuni watatusaidia na dunia nzima inatusaidia. Mwanzo ndio ufanisi. Tuna ari imara ya kwenda mbele kuelekea nuru.


Nguzo tatu za ahadi

Kwanza, hatua tuliyochukua leo inanuia inahusiana moja kwa moja na haki, utu, maisha na fahari ya kitaifa ambayo ni matakwa ya kitafia. Tunakusudia kudhihirisha haki zetu za uhuru. Tutafuata njia nyofu bila kuwekengeusha binadamu wenzetu.

Pili, Tutatangaza matakwa na maombi yetu mpata mtu wa mwisho afe na wakati wa mwisho afike.

Pili, kila mmoja na kila mtu aonyeshe mwisho wa matakwa ya haki na hamu ya watu wetu.

Tatu, kila kitendo kifanyike kwa kuzingatia utaratibu. Madai na misimamo wetu inatakiwa kutekelezwa kwa kuzingatia haki zote na moyo wa ukunjufu.

Tunatangaza Azimio hili la Uhuru tarehe mosi mwezi wa Machi mwaka wa 4252 tangu nchi yetu iasisiwe.

Wanaowakilisha taifa zima la Korea

Son Pyong-hui, Kil Son-ju, Yi Pil-chu, Paek Yong-song, Kim Wan-gyu, Kim Pyong-jo, Kim Chang-jun, Kwon Tong-jin, Kwon Pyong-dok, Na Yong-hwan, Na In-hyop, Yang Chon-baek, Yang Han-muk, Yu Yo-dae, Yi Kap-song, Yi Myong-yong, Yi Sung-hun, Yi Chong-hun, Yi Chong-il, Lim Ye-hwan, Pak Chun-sung, Pak Hui-do, Pak Tong-wan, Shin Hong-shik, Shin Sok-ku, O Se-chang, O Hwa-yong, Chong Ch¡¯un-su, Choe Song-mo, Choe Rin, Han Yong-un, Hong Pyong-gi, and Hong Ki-jo